Jumamosi, Agosti 03, 2013

MBARONI KWA KUKUTWA NA NGOZI YA CHUI KATAVI

Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Chelehani Kulwa 33 mkazi wa kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kukamatwa na nyara za serikali ngozi ya chui



Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema mtuhumiwa alikamtwa hapo Agosti 1 mwaka huu majira ya saa tisa na nusu alasiri nyumbani kwake akiwa na ngozi hiyo ya chuwi
Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa alikamatwa na nyara hiyo ya Serikali kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi la polisi kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijishughulisha na uwindaji haramu na amehifadhi ndani ya nyumba yake ngozi ya chuwi
Baada ya taarifa hizo kutoka kwa raia wema jeshi la polisi lilianza uchunguzi wa kumfuatilia mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho cha Kapanga
Kidavashari alieleza kuwa ndipo siku hiyo ya tukio polisi walipokwenda kumpekua mhuhumiwa Chelehani nyumbani kwake na kumkuta na ngozi ya chuwi yenye thamani ya shilingi milioni 5.670,000 kinyume cha sheria
Alisema mtuhumiwa baada ya mahojiano na jeshi la polisi alikiri kumiliki nyara hiyo ya Serikali kinyume na taratibu za sheria ya nchi
Upelelezi wa tukio hili umeisha kamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema wiki ijalo ili aewze kujibu shitaka la kukamatwa na nyara za serikali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo inakataza mtu binafusi kumiliki nyara za Serikali

0 comments:

Chapisha Maoni