Ofisi zaidi ya 12 za mabalozi wa Marekani katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini zimefungwa.
Hatua hiyo inafuatia serikali ya Marekani kusema Ijumaa kwamba inaamini kuwa al-Qaeda au kundi linaloshirikiana na al-Qaeda huenda likawa linapanga mashambulio.
Ubalozi wa Marekani mjini Kabul piya umefungwa kwa sababu ya ilani hiyo kuhusu usalama.
Mataifa kadha ya Ulaya nayo yamefuata - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema kuwa balozi zao mjini Sanaa, Yemen, zitafungwa mwisho wa juma.
0 comments:
Chapisha Maoni