Jumatano, Juni 07, 2017

MSIMAMO WA SERIKALI KATIKA MATUMIZI YA VX NA V8

Serikali imesema matumizi ya magari aina ya Toyota Land Cruiser VX kwa viongozi wake wa ngazi mbalimbali kwa Tanzania Bara yataendelea na haina mpango wa kutumia Toyota Prado kwa sasa kama ilivyo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Msimamo huo umewekwa wazi leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, wakati akijibu swali la mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa aliyehoji ni kwanini serikali isitumie Prado badala ya VX ili kuokoa fedha kutokana na gharama za ununuzi na matengenezo kwa VX kuwa juu kuliko Prado.
Kwa mujibu wa Mwambalaswa, gari moja aina ya VX inanunuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 220, wakati Prado inanunuliwa kwa shilingi milioni 120 na endapo serikali itanunua magari 200 ya Prado badala ya VX itaweza kuokoa shilingi bilioni 2 ambazo zinaweza kutatua kero ya maji katika jimbo lake la Lupa.

0 comments:

Chapisha Maoni