Jumatano, Machi 08, 2017

WAZIRI UMMY AKEMEA MA-DC A RC KUWAWEKA MAHABUSU MADAKTARI

Katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani,Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,amepiga marufuku wakuu wa mikoa na Wilaya (RC and DC) kuwadhalilisha kwa kuwasweka lupango au kuwasumbua madaktari ktk mikoa na Wilaya zao.
Waziri Ummy anasema kwa sasa imekuwa kama "fashion" kwa RCs na DCs kuwakamata watumishi wa umma na hasa madaktari na kuwaweka ndani bila sababu zenye mashiko,kiasi kwamba imeshusha morali ya kazi kwa watumishi hao wa afya au wale walio chini yao.
Mh.Ummy anasema jukumu hilo si lao kisheria,hivyo wanapaswa kuliacha mara moja,waziri amesisitiza kuwa ameshakubalina na Waziri wa TAMISEMI kuwaelekeza wakuu wa Wilaya na Mkoa mipaka yao ya kazi ili wasiingilie kazi na taratibu zilizo nje ya majukumu yao.
Yeye kama Waziri wa Afya,hakuwa tayari kuona madaktari wakinyanyaswa na kusumbuliwa na Wakuu wa mikoa na Wilaya bila sababu.
Agizo hili limekuja siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Singida Dr Nchimbi kumuweka ndani DMO wa Singida,kitu kilichosababisha Daktari huyo kuandika barua ya kujiuzulu na kuacha kazi.
Huko Arusha,RC Gambo hivi karibuni,alionekana ktk vyombo vya habari akimfokea na kumshutumu Daktari kwa makosa ambayo sio yake moja kwa moja.
Huko Lindi,Wilaya ya Kilwa,DC wa Wilaya hiyo,Mh.Ngubiagayi alimdhalilisha Daktari mbele ya vyombo vya habari kwa kuamuru polisi wamshikirie kwa kosa asilohusika nalo moja kwa moja,kitu kilichosababisha chama cha Madaktari Tz,kuweka katazo la kupewa ushirikiano kwa kiongozi huyo popote pale Tz.
Kwa kauli hii ya Waziri mwenye dhamana,akishirikiana na Waziri wa TAMISEMI,bila shaka wakuu wa Mikoa na Wilaya,watajua mipaka yao na kuheshimu taaluma za watu na kufuata misingi ya kanuni,sheria na taratibu na si kukurupuka mbele ya kamera ili waonekane kwenye TV.

0 comments:

Chapisha Maoni