Jumatano, Machi 08, 2017

RIPOTI KUHUSU HAKI ZA WANAWAKE AFRIKA YAZINDULIWA

Umoja wa Afrika, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa na ofisi inayoshughulikia mambo ya wanawake wamezindua ripoti kuhusu haki za wanawake barani Afrika, ikionyesha mafanikio yaliyopatikana kwenye haki za wanawake na changamoto zilizopo.
Mshauri maalum wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw Jean Mfasoni, amesema maendeleo yamepatikana kwenye kuwawezesha wanawake na mambo ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kujumuishwa kwenye vipengele vya makubaliano ya Maputo kuhusu haki za wanawake. Ripoti zimetaja mafanikio zaidi kwenye ushiriki wa wanawake kwenye siasa.
Hata hivyo ripoti imesema kuna pengo kubwa kwenye baadhi ya maeneo yanayohitaji hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na elimu ya kijinsia na afya ya uzazi, wanawake albino, ukatili wa kingono na kijinsia, matendo mabaya, sheria baguzi kwa wanawake, amani, usalama, na wanawake walio magerezani.

0 comments:

Chapisha Maoni