Jumatatu, Machi 06, 2017

MASHAMBA MAKUBWA YA BHANGI YATEKETEZWA MBEYA, WATUHUMIWA WENGINE WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA

Katika Operesheni na Misako inayoendelea kuhusiana na watu wanaojihusisha na usafirishaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata watu wawili wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya [Mateja] ambao ni 1.  EDSON MWANGOKA [32] Mkazi wa Mama John na 2. ABRAHAM EZEKIA [20] Mkazi wa Airport.
Aidha katika Oparesheni hiyo walikamatwa watu sita wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi ambao ni;

1. GWAMAKA SHWAIBU [30] Mkazi wa Mwakibete 
2. LAZARO AFRIKA [30] mkazi wa Ngyeke 
3. DAUDI MSOMA [30] mkazi wa mbalizi 
4. JOSEPH MWAMBUNGU [23] mkazi wa Sistila 
5. JOHN MNANDI [28] mkazi wa Sistila 
6. DAVID PROTAS [20] mkazi wa Sistila

Bhangi yenye jumla ya uzito wa gram 535 ilikamatwa. Watuhumiwa ni wauzaji wa dawa za kulevya na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 04.03.2017 lilifanya Oparesheni dhidi ya dawa za kulevya. Oparesheni ilifanyika huko katika milima ya Mbeya, kijiji cha Ihombe na katika milima ya Uwanji, iliyopo Kata ya Chimala tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali.
Katika Oparesheni hizo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata mashamba makubwa ya Bhangi. Shamba la bhangi lenye ukubwa wa ekari tatu lilikamatwa katika Kijiji cha Ihombe likiwa limelimwa Bhangi pamoja na mahindi. Pia shamba la Bhangi lenye ukubwa wa robo ekari likiwa limelimwa bhangi pamoja na mahindi lilikamatwa katika milima ya Uwanji Wilaya ya Mbarali.
Mashamba yote ya Bhangi yaliteketezwa kwa kuchomwa moto. Msako unaendelea kuwatafuta wamiliki wa mashamba hayo kwani katika Oparesheni hizo walikimbia na kutelekeza mashamba hayo.

0 comments:

Chapisha Maoni