Jumatatu, Machi 06, 2017

KENYA KUTOA PESA KWA WAFUGAJI ILI KUNUSURU MIFUGO YAO NA NJAA KALI

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itatumia dola za Kimarekani milioni 2.15 kwa ajili ya kuwapa wafugaji kununua chakula cha mifugo hadi ukame mkali utakapomalizika.
Msemaji wa Ikulu ya Kenya Bw Manoah Esipisu amewaambia wanahabari kuwa rais Uhuru Kenyatta atazindua rasmi malipo kwa ajili ya wafugaji walioathirika wa kaunti za Mandera, Marsabit, Isiolo, Tana River, Turkana na Wajir, huku serikali ikichukua hatua zaidi kupunguza ukame.
Wakati huohuo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yupo Nairobi kwa ziara ya siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya kikanda kufuatia njaa kuikumba kanda hiyo. 
Kwa mujibu wa taarifa wanadiplomasia wa ngazi ya juu watakutana na maofisa wa ngazi ya juu wa Kenya baada ya ukame kuwafanya zaidi ya Wakenya milioni 3 wakabiliwe na ukosefu mkubwa wa chakula.

0 comments:

Chapisha Maoni