Kanisa katoliki nchini Marekani limezuia kuchukuliwa hatua ya kisheria ya watu waliobakwa na makasisi.
Ripoti kutoka Marekani zinasema
kuwa, Kanisa Katoliki lilizuia kupasishwa sheria ya kuwakamata na
kuwafungulia mashtaka makasisi watakaopatikana na hatia ya kuwabaka watu
hususas watoto wadogo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa, kanisa
hilo lilifanya kila lililoweza kuzuia muswada uliokuwa umewasilishwa
Bungeni ambao kama ungepasishwa na kuwa sheria, basi ungewafuatilia
kisheria makasisi wa kanisa hilo watakaokabiliwa na tuhuma za ubakaji
hususan watoto wadogo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kupasishwa
sheria hiyo kungekuwa na ahueni kubwa kwa wahanga wa vitendo vya ubakaji
vinavyofanywa na makasisi wa kanisa katoliki nchini Marekani, vitendo
ambavyo vimeripotiwa kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni.
Katika kuhalilishwa kutopasishwa kwa sheria hiyo kanisa hilo limedai
kwamba, kama sheria hiyo ingepasishwa ingekuwa na madhara makubwa ya
kifedha kwa taasisi zinazojuhusisha na masuala ya watoto.
Kashfa mbalimbali za kimaadili na
kifedha zilizoikumba Vatican na Kanisa Katoliki katika miaka ya hivi
karibuni zimekuwa zikigonga vichwa vya habari na kuwa gumzo kubwa
lisilokwisha duniani.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, kuna
mamia ya kesi za ubakaji na ulawiti zinazowakabili makasisi ambazo
zimerundikana katika mahakama za Ulaya na Marekani zikisubiri kufanyiwa
uchunguzi jambo ambalo kwa hakika limeshusha hadhi ya Kanisa Katoliki
ulimwenguni.
0 comments:
Chapisha Maoni