Jumamosi, Machi 11, 2017

FAMILIA ZA WAHANGA WA CHAPECOENSE KWENDA MAHAKAMANI

Moja kati ya habari zilizoushtua ulimwengu asubuhi ya  Novemba 29, 2016 ilikuwa ni habari-mpasuko kuhusu kikosi cha timu ya soka ya Chapecoense ya Brazil kupata ajali ya ndege wakiwa angani kuelekea kutua katika uwanja wa ndege wa Medellin.
Watu 71, wakiwemo wachezaji 19 na wahudumu wa klabu hiyo, walifariki katika ajali hiyo.
Jipya kuhusiana na kisa hicho cha mwishoni mwa mwaka jana ni familia za wachezaji wa timu hiyo kuwa na mpango wa kuipeleka klabu hiyo mahakamani, kwa madai kuwa hawajapewa fidia za kutosha kutokana na mkasa huyo wa Novemba 28.

0 comments:

Chapisha Maoni