Leo ni siku ya wanawake duniani na staa wa movie Tanzania na Mwanasiasa aliye kwenye vichwa vya habari daily Wema Sepetu leo ameamua kuadhimisha siku hii adhimu kwa wanawake mkoani Morogoro, unataka jua kafanya nini Morogoro? Katufahamisha kupitia account yake ya Instagram na hiki ndicho alichotuandikia
Leo ni siku ya wanawake Duniani, na kama mwanamke nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabili ya Maji... Wote tunajua kuwa mwanamke ndo anaekerwa zaidi katika upatikanaji wa maji... Labda haitotusaidia leo wala kesho, lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu hapo baadae.... Morogoro ni eneo linalosadikika kuwa Chanzo cha Maji hata yale tunayotumia Mkoani kwetu (Daressalaam)... Ninajiskia faraja kuwa kutakuwa na helping hand yangu somewhere when it comes to Water supply in my society... Mazingira yetu hayana Itikadi wala Vyama, Yanagusa kila mtu... I feel honored to be part of this activity... Tumetoka Kata ya Kilakala and now tunaelekea kwenye Chanzo kingine kinachoitwa Mambogo....
0 comments:
Chapisha Maoni