Watu zaidi ya 130,000 kaskazini mwa
jimbo la California wametakiwa kuhama makazi yao baada ya bwawa refu
zaidi Marekani kukabiliwa na hatari ya kubomoka.
Mtaro wa kupitisha maji wakati wa dharura katika bwawa la Oroville unaweza kuporomoka wakati wowote, maafisa wamesema.
Mtaro huo umedhoofishwa sana na mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.
Wahandisi
waligundua kwamba vipande vikubwa vya saruji vilikuwa vimebambuka
kutoka kwenye mtaro wa kuondosha maji kwenye bwawa hilo.
Watu wanaoishi katika maeneo ambayo huenda hakakumbwa na amfuriko bwawa hilo likiporomoka wametakiwa kuhama mara moja.
Viwango
vya maji katika bwawa hilo vimepanda sana kutokana na mvua kubwa pamoja
na theluji, baada ya miaka mingi ya kiangazi Valifornia.
Ni mara ya kwanza kwa Ziwa Oroville kukumbwa na dharura ya aina hiyo katika miaka 50 tangu kujengwa kwa bwawa hilo.
Idara
ya maji na maliasili katika jimbo la California ilisema Jumapili kwamba
inaachilia karibu futi 100,000 mche mraba (mita 2,830 mche mraba)
kila sekunde kupitia mtaro mkuu wa kuondosha maji kwenye bwawa hilo
kujaribu kupunguza kiwango cha maji kwenye bwawa hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni