Jumamosi, Aprili 02, 2016

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LINAKULETEA HUDUMA HII MPYA MLANGONI KWAKO

SHIRIKA la Posta Tanzania linatarajia kuzindua huduma mpya POSTA MLANGONI ambapo kila mwananchi atapelekewa kufurushi, taarifa au bidhaa zilizotumwa kwa kupitia Ofisi za Posta.
Hayo yamesemwa na Kaimu Posta Master Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Shirika hilo litaanza na kata 48 ya Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar Unguja kata 2 na Pemba kata 4.
Kapinga amesema kuwa kata za Tanzania bara zilizopo katika jiji la Arusha ni 8 Mkoa wa Dodoma ni kata 8 na jijini Dar es Salaam ni kata 32.
''Tumeanza na kata 48 kwa kuwa kata hizo zimekamilika miundombinu yake" amesema Kapinga.
Amesema kuwa awamu ya kwanza itaanza hapo April 5 na awamu ya Pili itakuwa katika mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mara, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Pwani, Manyara, Simiyu na Geita kwa upande wa Tanzania visiwani itakuwa ni Unguja na Pemba.
Na awamu ya Tatu watamalizia na mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Kigoma, Singida, Rukwa, Ruvuma, Katavi na Njombe amesema kuwa shirika la Posta Tanzania lina masanduku 173,000 yaliyosimikwa na shirika hilo na ofisi 172.

0 comments:

Chapisha Maoni