WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amewataka
wananchi wa Zanzibar waondoe hofu kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu
visiwani humo. Akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo na wananchi
hao wakati alipokuwa anatembelea mitaa mbalimbali ya Soko Kuu la mjini
Chake Chake, Pemba aliwataka wananchi hao waendelee na shughuli zao za
kujipatia kipato kama kawaida na hakuna mtu atakayewabughudhi kwani
ulinzi umeimarishwa, na waachane na uzushi wa kutokea vurugu unaoenezwa
visiwani humo.
Waziri Kitwanga alianza matembezi hayo mitaani
mara baada ya kufanya mazungumzo na Kamati ya Ulinzi na Usalama mjini
Chake Chake ambapo walimuhakikishia kuwa, Pemba yote ni salama na ulinzi
umeimarishwa na hakuna atakaye fanyiwa vurugu kwa mtu yeyote
atakayefuata sheria.
Waziri Kitwanga aliwataka wananchi hao kuondoa hofu wanapowaona askari mbalimbali wakipita mitaani kwani wapo kwa ajili ya kuwalinda wananchi hao pamoja na mali zao katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.
Waziri Kitwanga aliwataka wananchi hao kuondoa hofu wanapowaona askari mbalimbali wakipita mitaani kwani wapo kwa ajili ya kuwalinda wananchi hao pamoja na mali zao katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.
“Musiwaogope askari, na wala msiwe na wasiwasi, mnapowaona shangilieni
kwani askari ndio msaada wako kwa ajili ya usalama wako endapo
inapotokea vurugu ya aina yoyote, mtaenda kupiga kura salama na mtarudi
salama, hakuna mtu wa kuwabughudhi, msitishwe na mtu yeyote,” alisema
Waziri Kitwanga na kufafanua;“Leo nazunguka mitaa mbalimbali ya hapa
Pemba, lengo ni kuchukua maoni yenu pamoja na kuwaondolea hofu wananchi
na kuwahakikishia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri
kwa ajili ya kulinda usalama, hivyo jitokezeni kwa wingi siku ya
uchaguzi mkapigie kura kiongozi mnaemtaka.”
Hata hivyo, Waziri
Kitwanga alifanya ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba katika msitu wa Ngezi
unaodaiwa kuwa kuna baadhi ya wakimbizi wamejificha katika msitu huo ili
kuokoa maisha yao baada ya kudaiwa kuwa kutatokea na vurugu. Kitwanga
akiongozana na Wakuu wa Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba pamoja
na maafisa wa Jeshi la Polisi Pemba, walienda katika msitu huo na
kuukagua na hawakukutana na mtu hata mmoja aliyejificha msituni humo
kama inavyodaiwa na kusambazwa habari na baadhi ya watu wasioitakia mema
Zanzibar.
“Ndugu waandishi wa habari, tumezunguka kwa pamoja
kuungalia msitu huu, kuwatafuta hao wakimbizi, hatujamuona mtu yeyote,
ukisikia propaganda ndio hii, watu hawaitakii mema Zanzibar na Tanzania
kiujumla, mmeona kuwa habari hii ni ya uongo, hakuna mkimbizi yeyote
katika msitu huu kama tulivyoshuhudia wote kwa ujumla,” alisema Kiwanga.
Aliongeza kuwa, baadhi ya wananchi ambao wana mipango yao binafsi
wanawatia hofu wananchi kwa kutunga habari za uongo kuwa Zanzibar
imechafuka, wakati habari hizo hazina uhalisia wowote.
Hata hivyo, wananchi wa Pemba walimuhakikishia Waziri Kitwanga wanafanya shughuli zao za kuwapatia kipato kama kawaida na pia siku ya uchaguzi wataenda kupiga kura kama kawaida kwani wanaamini amani itakuwepo kama ilivyokuwa sasa.
Hata hivyo, wananchi wa Pemba walimuhakikishia Waziri Kitwanga wanafanya shughuli zao za kuwapatia kipato kama kawaida na pia siku ya uchaguzi wataenda kupiga kura kama kawaida kwani wanaamini amani itakuwepo kama ilivyokuwa sasa.
Waziri Kitwanga alifanya ziara Zanzibar katika Kisiwa cha
Unguja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wakuu wa Vyombo
vya Ulinzi na Usalama, na baadae kumalizia ziara yake kwa kutembelea
katika mikoa yote ya Pemba ikiwa ni hatua ya kuangalia hali ya usalama
visiwani humo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu katika maeneo hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni