Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) lilisema kuwa idadi
ya watu waliokimbia kutoka nchi ya Burundi na kutafuta makazi katika
nchi jirani ni zaidi ya 250,000,msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema siku
ya Ijumaa (Jana).
"Idadi ya wakumbizi wapya kutoka Burundi na
kuelekea nchi jirani kwa wiki imekuwa zaidi ya 1,000 nchini Tanzania,
500 nchini Uganda, 230 nchini Rwanda na 200 katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo,"Farhan Haq, naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa,
alisema katika habari za kila siku.
Shirika la Umoja wa Mataifa
pia lilisema kuwa ingawa kumekuwa vurugu kidogo hivi karibuni,wakimbizi
wanaowasili katika nchi hizo wanaripoti ukiukaji wa haki za binadamu
nchini Burundi,aliongeza.
0 comments:
Chapisha Maoni