Takriban wanafunzi 38 walijeruhiwa siku ya Ijumaa (Jana) katika kukanyagana ambayo ilisababishwa na hofu ya ghafla katika Chuo Kikuu cha Kenyatta Kaunti ya Kiambu.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kiambu, James Mugera, alisema wanafuzi katika chuo hicho walidhania mapambano kati ya wanafunzi wawili katika maktaba yalikuwa mashambulizi ya kigaidi, karibia saa sita mchana na pia akathibitisha idadi ya waliojeruhiwa.
Alisema kuwa wanafunzi walikuwa wakijaribu kukimbilia usalama ambapo wengine waliruka kutoka gorofa ya juu na kusababisha majeraha yao.
0 comments:
Chapisha Maoni