Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai -ICC, ya huko The Hague nchini Uholanzi, imemhukumu jela miaka 40, aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa Waserbia wa Bosnia, Radovan Karadzic, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica.
Radovan karadzic pia anakabiliwa na hukumu zingine tisa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, pale alipowalenga, raia wengi wa jamii ya kiislamu, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sarajevo miaka ya tisini.
Hili ni hitimisho la kesi ndefu tangu miaka 7 iliyopita. Radovan Karadzic alikamatwa mwaka 2008 wakati alikuwa mafichoni katika mji wa Belgrade. Baada ya miaka kumi na moja akiwa mafichoni, alifikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Radovan Karadzic ataendelea kuzuiliwa na Mahakama kwa kusubiri kukamilika kwa maelezo kuhusu kuhamishwa kwake katika nchi nyingine ambapo atatumikia adhabu yake.
Mtuhumiwa huyo tayari ametangaza kwamba atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.
0 comments:
Chapisha Maoni