Jumatatu, Machi 21, 2016

MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR KATIKA MAJIMBO MATANO HAYA HAPA

Kwa mara nyingine jana Zanzibar historia ilitengenezwa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa marudio, hii ni baada ya ule wa awali wa oktoba 25 mwaka jana kufutwa kufuatia kuwa na changamoto nyingi ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC, bwana Jecha kama ambavyo Fichuo iliwahi kukuripotia.
Ni vema kuashiria hapa kwamba chama cha Wananchi CUF kiliususia uchaguzi huu wa marudio lakini vyama vingine vyote vya upinzani vinavyosalia vimeshiriki.
Sasa matokeo ya awali ya Urais kwa Majimbo ya OLE, Ziwani, Chonga, Wawi na Chake yametoka
huku yakionesha kuwa Dkt. Ali Mohamed Shein anaongoza.

0 comments:

Chapisha Maoni