Jumatano, Machi 30, 2016

MARUFUKU KUTUMIA WATOTO KATIKA SHEREHE ZAIDI YA SAA 12 JIONI MBEYA

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kupitia dawati la Jinsia na watoto limepiga marufuku wazazi kuruhusu watoto wao wadogo kushiriki katika sherehe ambazo zinafanyika katika muda unaozidi saa kumi na mbili jioni.
Hii ni kwaajili ya kuwalinda na maadili yasiyofaa lakini pia kuwapa watoto haki yao ya msingi ya kupumzika.
Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kuchukua hatua kali kwa wale watakao kaidi katazo hilo ikiwa ni pamoja na sherehe husika kuharibika lakini pia kuwachukulia hatua wote walioruhusu uwepo wa watoto katika sherehe hizo.

0 comments:

Chapisha Maoni