Alhamisi, Machi 24, 2016

KIKONGWE AUAWA KWA MAPANGA MBOZI, MBEYA

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Isandula kata ya Kilimampimbi wilayani Mbozi mkoani Songwe ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofamika.
Diwani wa kata ya Kilimampimbi Henry Mwilenga akizungumza kwa njia ya simu amemtaja marehemu kuwa ni Luka Kabuka anayekadirwa kuwa na umri wa kati ya miaka 70-80 mkazi wa Isandula wilayani humo
Mwilenga amesema tukio hilo limetokea Machi 21 saa mbili usiku mwaka huu ambapo marehemu alikuwa akitokea matembezini na kabla hajafika nyumbani kwake mita sabini alivamiwa na watu wasiofahamika na kufanyiwa unyama huo.
Amesema tukio hilo limegunduliwa na mtoto wa marehemu ambaye naye siku ya tukio alichelewa kufika nyumbani na wakati anafika karibu na eneo la tukio ndipo aligunduwa kuwa aliyeuawa ni baba yake na ndipo akapiga mayowe na kuomba msaada.
Mwilenga amesema baada ya tukio hilo kutokea waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka hospitali ya wilaya ya Mbozi kwaajili ya uchunguzi na kusadikiwa kuwa marehemu alinyofolewa baadhi ya viungo na wakuruhusiwa kwa ajili ya mazishi.
Katika hatua nyigine diwani huyo amesema marehemu ameuawa kinyama kwani alipoiangalia maiti ilikutwa na majereha makubwa matano usoni hali inayoashiria kuwa alipigwa na vitu vyenye ncha kali.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwagundua watu waliohusika na unyama huo kwani tukio hilo ni la pili kutokea katika kata hiyo ndani ya miaka miwili.
Kwa upande wake mgaga mkuu wa wilaya ya Mbozi Isaac Ibrahim akizungumzia suala hilo amekana kuwa hana taarifa ya tukio hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni