Jumatatu, Februari 08, 2016

WASICHANA MILIONI 200 WAMEKEKETWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kwenye ripoti yake kwamba kina mama na wasichana wasiopungua milioni 200 katika nchi 30 wamepashwa tohara.
Ripoti yake hiyo imetolewa Jumamosi wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya kupinga ukeketaji dhidi ya wanawake.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanawake hao wanakeketwa nchini Indonesia, Egypt na Ethiopia pekee.

0 comments:

Chapisha Maoni