Jumanne, Februari 02, 2016

WAKE WA MARAIS AFRIKA WATAKA KUTOKOMEZWA UKIMWI

Wake wa marais wa nchi za Afrika wamesisitizia umuhimu wa kuzidishwa juhudi za kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Wake wa marais wa Afrika wamesema hayo kupitia muungano wao unaojulikana kama Organization of African First Ladies against HIV/AIDS (OAFLA) ambapo wamesema maambukizi mapya ya virusi vya HIV kwa watoto wachanga ni jambo linalotia wasiwasi na kwamba suhula zaidi zinahitajika kwa ajili ya kukabiliana na hatari hiyo.
Wake hao wa marais wa Afrika ambao wamekutana mjini Addis Ababa, Ethiopia wameelezea kusikitishwa na ripoti za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya HIV yanaonekana kukithiri mno miongoni mwa wanandoa.
Michel Sidibe, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) amesema azma ya kuangamiza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030 bado inaweza kufikiwa endapo maamuzi mazuri na ya busara yatachukuliwa haraka.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), watu milioni 37 wanaishi na virusi vya HIV na kati ya hao, milioni 26 wanatoka barani Afrika.

0 comments:

Chapisha Maoni