Tabasamu ni ishara ya afya nzuri, furaha na utulivu. Si kama tu inakusaidia kuwa na amani, bali pia inaonesha kwamba wewe ni mtu mwema unayependa kuwasaidia wengine.
Tulizaliwa na uwezo wa kutabasamu au tulijifunza?
Baadhi ya watu wanaamini tulijifunza, kwa sababu tunajaribu kutoa tabasamu mara kwa mara ili kuanzisha uhusiano mzuri na wengine. Wahudumu wa ndege na wafanyakazi wanaoshughulikia uhusiano wa umma wanafanya mazoezi sana ili kutoa tabasamu ya kuvutia zaidi, na wamefanikiwa.
Lakini utafiti mpya pia unaonesha kuwa uwezo wa kutabasamu unaamuliwa na jeni zetu. Ni vigumu kwa mtu asiyerithi jeni husika kutoa tabasamu, na watoto na wazazi wao huwa na tabasamu zinazofanana. Bila shaka hii ni matokeo ya urithi.
Tabasamu inarithiwa, lakini haimaanishi kwamba huwezi kujifunza kutabasamu. Wataalamu wa elimu na saikolojia wanaona binadamu wanaweza kujifunza kitu chochote. Hivyo ukitaka kuwa na tabasamu inayowavutia wengine, unahitaji kufanya mazoezi kwa bidii.
Tabasamu itakusaidia katika maisha na kazi zako.
CRI
0 comments:
Chapisha Maoni