Watu watatu walifariki na wengine 38 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi walipokuwa wakifanya ibada chini ya mti katika mkoa wa KwaZulu-Natal, nchini Afrika kusini hapo jana (Jumamosi).
Wanawake watatu wenye umri kati ya miaka 50 na 65 walifariki papo hapo huku wengine wakinusurika na majeraha na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu. Serikali imeonya wananchi dhidi ya kukaa chini ya miti wakati kuna mawingu mazito. Milipuko ya radi ni kawaida katika maeneo ya mashariki na kaskazini ya Afrika kusini kati ya mwezi wa Oktoba na Mechi.
0 comments:
Chapisha Maoni