Abiria wengi wa ndege wanalalamikia ladha mbaya ya vyakula kwenye ndege. Wahudumu wa ndege pia hawajui chanzo cha hali hiyo, kwa sababu vyakula vyote vimeandaliwa kwa makini, ili kukidhi mahitaji ya abiria. Hivi karibuni watafiti wanabainisha kuwa kelele ndani ya ndege zinawafanya abiria kusikia kama vyakula vina ladha mbaya.
Utafiti unaonesha kuwa mchakato wa kula unaweza kuathiriwa na mazingira, kwa mfano kelele zinaweza kuathiri hisia ya kuonja ya binadamu. Kufuatia ongezeko la kelele, uwezo wa kuonja ladha tamu na chachu ya chakula unapungua. Hivyo, wataalamu wanashauri watu wasichague mkahawa wenye kelele nyingi. Muziki laini unaweza kuongeza utamu wa chakula.
Mbali na hayo, kelele pia zinaweza kuharibu uwezo wa kusikia wa binadamu, kuvuruga mapigo ya moyo, kuleta wasiwasi na kuongeza mapigo ya moyo na shinikizo la damu.
0 comments:
Chapisha Maoni