RAPA ‘grade one’, Kanye West hatimaye ameonesha kweli kuzima bifu na rapa mwenzake Wiz Khalifa baada ya kuliweka jina jipya la albamu yake ijayo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliutumia kuachia baadhi ya posti zake huku akiwaweka mashabiki wazi kuwa tayari ameshakamilia albamu yake ya The Life Of Pablo (T.L.O.P) sambamba na kuziweka wazi baadhi ya nyimbo zitakazokuwepo.
Wiki chache zilizopita, Kanye aliingia bifu na Wiz kuhusiana na jina la albamu ambalo Kanye alilibadilisha kutoka Swish na kuwa Waves kitendo ambacho Wiz alikuwa na idea hiyo na pia ndiyo wazo la rafiki yake kipenzi wa zamani aliyejulikana kama Max B.
0 comments:
Chapisha Maoni