Jumanne, Februari 23, 2016

KILICHOAMULIWA MBEYA KUHUSU KODI

MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameziagiza halmashauri zote za Wilaya na jiji kuelekeza nguvu katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya ndani ili kuondokana na utegemezi na kufikia matarajio ya wananchi.
Akizungumza katika ufunguzi wa  kikao cha  kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), cha mwelekeo ya bajeti ya fedha kwa mwaka  2016/2017 amesema halmashauri za mkoa wa Mbeya zimekuwa tegemezi kwa kiwango kikubwa.
Amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa  utegemezi wa juu wa halmashauri hizo ni asilimia 97 na utegemezi wa chini ni asilimia 76 na hivyo uendeshaji wake kutegemea fedha kutoka nje.
Kandoro ambaye  ni mwenyekiti wa kamati ya RCC amesema kuwa matarajio ya wananchi hayawezi kufikiwa bila halmashauri kuelekeza nguvu kwenye ukusaji wa mapato.
Amesema uwezo wa halmashauri katika kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, miundombinu na maji unategemea na mapato ya ndani yanayokusanywa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya ushauri kutoka mkoa wa Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine kinatarajia kujadili masuala mbalimbali pamoja na kuyawekea maazimio.

0 comments:

Chapisha Maoni