Alhamisi, Februari 04, 2016

DEREVA WA GARI UNAPASWA KUYAKUMBUKA HAYA

Gari linapokuwa katika mwendokasi wa:-

1) 30Kph litahitaji umbali wa mita 12 liweze kusimama (sawa na umbali wa kuyapita magari 3). Kati ya hizo mita 12; mita 6 ni za kufikiri na kuchukua hatua (reaction time) na zingine mita 6 ni za kusimama (breaking time).
2) 50Kph litahitaji umbali wa mita 23 ili kuweza kusimama (sawa na umbali wa kuyapita magari 6). Kati ya hizo mita 23; mita 9 ni za kufikiri na kuchukua hatua (reaction time) na zingine mita 14 ni za kusimama (breaking time).
3) 80Kph litahitaji umbali wa mita 53 ili liweze kusimama (sawa na umbali wa kuyapita magari 13). Kati ya mita hizo 53; mita 12 ni za kufikiri na kuchukua hatua (reaction time) na zingine mita 41 ni za kusimama (breaking time).
4) 100Kph litahitaji umbali wa mita 73 kusimama (sawa na umbali wa kuyapita magari 18). Kati ya hizo mita 73; mita 16 ni za kufikiri na kuchukua hatua (reaction time) na mita zingine 57 ni za kusimama (breaking time).
5) 112Kph litahitaji umbali wa mita 96 ili liweze kusimama (sawa na umbali wa kuyapita magari 24). Kati ya hizo mita 96; mita 21 ni za kufikiri na kuchukua hatua (reaction time) na mita zingine 75 ni za kusimama (breaking time).
KUMBUKA KWAMBA: Uwezo wa gari kusimama haraka au kwa kuchelewa zaidi utategemea hali njia, hali ya hewa, uwezo binafsi wa MTU (dereva) kufikiri kwa kasi na kuchukua hatua bila kupanic na hali ya gari lenyewe.
Umbali uwiano huu wa mwendokasi na uwezo wa gari kusimama ni wa kitaalamu na umethibitishwa kisayansi.
Hata kwenye usafiri wa Ndege, urefu wa Uwanja wa Ndege (Runway) ndio huamua ni aina gani ya ndege zinaweza kutua na kupaa katika uwanja huo. Jinsi njia ya kutua na kupaa (Runway) inapokuwa ndefu ndivyo ndege kubwa na zenye kasi zaidi zinaweza kutua na kupaa. Usishangae kuna baadhi ya ndege hazitui baadhi ya viwanja au/na kama zitatua zinaweza kupata ajali kwa kuwa zitamaliza uwanja kabla ndege haijafika katika speed ya kusimama au kupaa. Hata gari nalo lina vigezo vyake.
WITO WANGU KWAKO: Usikimbie tu hovyo barabarani ati kwa kuwa injini ya gari lako ni kubwa na ya kisasa.
Kalakabhaho yakikukuta majanga usitafute mchawi fahamu kuwa mchawi ni wewe mwenyewe.
High Speed Kills - Mwendokasi Unaua.

0 comments:

Chapisha Maoni