Jumamosi, Januari 23, 2016

YANGA SI SHWARI

Baadhi ya wanachama wameandamana hadi makao makuu ya Klabu kupinga kujiuzulu kwa aliyekuwa katibu mkuu Dr. Jonas Tiboroha huku wakimsihi kubadili maamuzi yake.
Inasemekana fukuto la mgogoro lilikuwepo toka muda ila leo ndipo limelipuka,chanzo kikubwa ni kundi la wanachama wa Yanga waliozoea kula hela za bure kupitia Yanga lakini toka uteuzi wa Dr . Jonas Tiboroha aliyeifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na kuziba mianya hiyo hivyo wanachama hao wenye sauti ndani ya Yanga wameamua kumsukia zengwe katibu huyo.
Moja ya tuhuma anazopewa Tiboroha na kundi linaloongozwa na Chanji ni kuwa katibu alisafiri kwenda Ghana kuhudhuria kongamano la shirikisho la FIFA bila idhini ya Mwenyekiti, Hivo hiyo ni tuhuma au angepaswa katibu kupongezwa?maana alihudhuria mafunzo ambayo yameongeza uweledi katika kuiongoza Yanga. .
Kikubwa tuiombea klabu yetu isiingie kwenye mgogoro mkubwa utakaopelekea mpasuko ila hali ni mbaya.

0 comments:

Chapisha Maoni