Jumatatu, Januari 18, 2016

WHO: TANZANIA HAIJAPATA SULUHU YA KIPINDUPINDU

Shirika la afya duniani (WHO) imeonya kuwa haijapatikana suluhu kamili kwa mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umekumba maeneo mbali mbali nchini Tanzania kwa muda wa miezi mitano sasa na kuua zaidi ya watu 200.
Rufaro Chatora, mwakilishi wa WHO nchini Tanzania amesema kuwa juhudi za maafisa wa afya kusitisha kusambaa kwa maambukizi hayo lazima ziende sambamba na kuimarisha hali ya usafi wa mazingira pamoja na kuelimisha umma kuhusu ugonjwa huo.
Zaidi ya visa 13,000 vya kipindupindu vimeripotiwa nchini hapa hadi sasa

0 comments:

Chapisha Maoni