Jumamosi, Januari 16, 2016

WANAFUNZI UINGEREZA WANAKABILIWA NA NJAA

Utafiti mpya umeonyesha kuwa wanafunzi wengi nchini Uingereza wanakabiliwa na baa la njaa kwa kuwa wazazi wao wameshindwa kuwalisha.
Utafiti huo uliofanywa na shirika la YouGov umebainisha kuwa, asilimia 80 ya walimu katika shule za Uingereza wanalazimika kuwanunulia wanafunzi wao kitu cha kula. Walimu hao wamesema wanalazimika kuwanunulia chakula wanafunzi haswa nyakati za asubuhi ili kuwazuia wasilale madarasani na pia kuwafanya wamakinike. Idadi kubwa ya wanafunzi waliohojiwa katika utafiti huo wamesema wazazi wao hawana uwezo wa kuwapa kitu cha kula asubuhi na hivyo kulazimika kwenda shuleni wakiwa na njaa. Wakati huo huo, Muungano wa Taifa wa Walimu Wanawake nchini Uingereza (NASUWT) umelaumu sera za kiuchumi na kijamii za serikali kutokana na hali hiyo inayowakabili wanafunzi nchini humo. Chris Keates, mwenyekiti wa muungano huo ameliambia gazeti la Daily Mirror kuwa, serikali ina jukumu ya kukabiliana na changamoto hiyo na wala sio kuongeza kiwango cha umaskini na watu kukosa makaazi.

0 comments:

Chapisha Maoni