Jumanne, Januari 26, 2016

UKOSEFU WA HEWA SAFI OFISINI WAATHIRI UWEZO WA KUAMUA

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard cha Marekani unaonesha kuwa mazingra ya ofisi yana uhusiano mkubwa na kazi. Kama mazingira ya ofisi ni mazuri, hali ya uchafuzi wa hewa na idadi ya carbon dioxide iko chini ya kiwango cha wastani, uwezo wa ufahamu, wa kumbukumbu wa kujifunza wa wafanyakazi utaongezeka kwa kiasi kikubwa, na ufanisi wa kazi wao utaongezeka kwa maradufu.
Watafiti waliwachagua washiriki 24 wa utafiti huo, ambao wanafanya kazi kwa siku sita katika mazingira tofauti. Washiriki hao walifanyiwa upimaji kuhusu upande wa kazi za msingi, kushughulikia msukosuko na kukusanya habari, halafu watafiti wakalinganisha uwezo wao wa kuamua.
Matokeo ya utafiti huo yanabainisha kuwa mazingira bora na safi ya ofisi yanaweza kuongeza uwezo wa kuamua wa wafanyakazi kwa asilimia 61. Mbali na hayo, watafiti pia wanasema, kukuza maua ofisini kunaweza kuongeza hamu na juhudi ya wafanyakazi na kuongeza ufanisi wa kazi kwa asilimia 15.

0 comments:

Chapisha Maoni