Alhamisi, Januari 14, 2016

TV YA AL-JAZEERA KUSITISHA MATANGAZO YAKE MAREKANI

Mtandao wa FICHUO leo hii umeinukuu kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar imesema kuwa itasimamisha matangazo yake nchini Marekani Aprili 30 mwaka huu, ikiwa ni chini ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake nchini humo.
Shirika hilo la habari limesema kuwa limelazimika kufunga matangazo yake kutokana na kutokuwepo soko la televisheni nchini humo. Al-Anstey, Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo amesema hawana budi kufunga matangazo ya runinga hiyo kwa kuwa mazingira ya biashara na hasa matangazo ya biashara nchini humo ni kinyume kabisa na matarajio yao. Mwaka 2013, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa al-Jazeera, Ehab al-Shihabi alisema kuwa runinga hiyo huwa na watazamaji kati ya elfu 20 na 40 wakati wa matangazo muhimu, kiwango ambacho ni kidogo mno ikilinganishwa na mashirika mengine ya runinga ya kimataifa. Shirika hilo lenye makao makuu Doha, Qatar limesema kuwa badala yake linaimarisha na kupanua huduma ya kimtandao katika maeneo ambayo yanaendesha mfumo huo kwa sasa. Hata hivyo wadadisi wa mambo wanasema kuwa, huenda kuporomoka kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa kumechangia Qatar kufunga kanali hiyo ya televisheni haswa ikizingatiwa kuwa uchumi wake unategemea pakubwa uuzaji wa mafuta.

0 comments:

Chapisha Maoni