Jumamosi, Januari 16, 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA- JUMAMOSI 16.01.2016

Meneja wa Liverpool, Jusrgen Klopp, 48, anasema 'alichombezwa' na Sir Alex Ferguson mwaka 2013 ili ajiunge na Manchester United, lakini akakataa jina lake kuwekwa kwenye orodha ya mameneja waliokuwa wakitafutwa na klabu hiyo (Daily Mirror), Klopp anasema hakuweza kuondoka Borussia Dortmund wakati huo kwa sababu ilikuwa katikati ya msimu (Sun), kiungo wa Liverpool amesisitiza kuwa mfumo wa mazoezi wa Klopp sio sababu ya timu hiyo kuwa na majeruhi wengi (Times), Liverpool huenda wakataka kumsajili Shane Long kutoka Southampton (Sun), Liverpool pia wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Inaki Williams, 21, ambaye pia anatazamwa na Atletico Madrid na Real Madrid (Guardian), Chelsea wanafikiria kumrejesha tena, meneja wa sasa wa Leicester City, Claudio Ranieri Stamford Bridge (Tuttosport), kiungo wa Chelsea Willian, 27, anataka kusaini mkataba wa muda mrefu (Sun), kiungo wa Newcastle, Jonjo Shelvey, 23, anafurahia changamoto mpya, baada ya 'kusikitishwa' akiwa Swansea (Wales Online), Manchester United wanamtaka mkuu wa ukocha na maendeleo ya wachezaji wa Tottenham, John McDermott, ili afundishe akademi ya Old Trafford (Times), Manchester City wanajiandaa kufanya mabadiliko makubwa wakimtarajia Pep Guardiola, kwa kumfuatilia John Stones wa Everton, huku Wilfried Bony na Eliaquim Mangala wakiondolewa (Daily Telegraph), meneja wa Everton, Roberto Martinez anasema Stones amepevuka kama mchezaji na kiongozi msimu huu na anaamini kutomuuza kwenda Chelsea mwaka jana kumemsaidia kukua (Daily Express), Everton watakabiliwa na ushindani kutoka West Ham na Newcastle katika kumsajili beki wa Leeds, Sam Byram (Guardian), Watford wana matumaini ya kukamilisha usajili wa winga Nordin Amrabat, 28 kutoka Malaga (Daily Star), mshambuliaji wa Lyon, Alexandre Lacazette, 24, anasema hatoondoka Ufaransa mwezi huu, lakini anaweza kuhamia England mwisho wa msimu, huku Chelsea na Newcastle wakimfuatilia (London Evening Standard), Southampton wamechelewesha majadiliano ya mkataba mpya na mshambuliaji wake Graziano Pelle, ambaye amebakiza miezi 18, na huenda akachukuliwa na Juventus au Fiorentina (Daily Echo), mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck, 25, na viungo Francis Coquelin, 24, na Jack Wilshere, 24, wamerejea mazoezini, lakini watarejea rasmi uwanjani baada ya wiki kadhaa (Independent), Swansea wamekataa dau kutoka Sunderland la kumsajili Andre Ayew, 26 (Daily Mirror).

SALIM KIKEKE

0 comments:

Chapisha Maoni