Jumamosi, Januari 16, 2016

TANZANIA YATAKA KUSTAWISHWA ZAIDI UHUSIANO NA IRAN

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania ametaka kuimarishwa uhusiano wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya utalii.
Nape Nnauye ameeleza kuridhishwa na kutiwa saini makubaliano ya kiutamaduni kati ya nchi mbili hizo na kubainisha kuwa kustawisha uhusiano wa sekta ya utalii kati ya Iran na Tanzania ni muhimu sana kwa nchi mbili hizo na amelipokea vizuri suala la kupewa mafunzo wasanii wa Tanzania nchini Iran.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania ameyasema hayo katika mazungumzo na Ali Bagheri mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni cha Iran jijini Dar es Salaam Tanzania.
Katika mazungumzo hayo Ali Bagheri, Mshauri wa Masuala ya Utamduni wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikifanya juhudi za kuimarisha amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla na kwamba urafiki na kuishi kwa maelewano ni moja ya vigezo vinavyopewa umuhimu mkubwa na Wairani.
Bagheri pia amesisitiza kuwa upo udharura wa kutengenezwa filamu ya pamoja ya kutoa mafunzo kwa wasanii na wamiliki wa vyombo vya habari na pia kwa ajili ya kustawishwa sekta ya utalii kati ya Iran na Tanzania.

0 comments:

Chapisha Maoni