Jumamosi, Januari 16, 2016

DAR ES SALAAM NA PWANI KUKOSA MAJI MASAA 36

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), Limetoa taarifa kwa wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na Mji wa Kibaha mkoani Pwani kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 36 kwa siku za Jumatatu 18/01/2016 na Jumanne 19/01/2016.
Mtambo wa Ruvu Juu utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi Kumalizia kazi za Ujenzi kwa kuunganisha Pampu za Mtambo mpya Mtoni. Zoezi hili linaashiria kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu juu. Shirika linakusudia kuzalisha maji mapya toka Mtambo wa Ruvu Juu kuanzia tarehe 28 Februali 2016 na Kuondoa kabisa tatizo la maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Juu
Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo yafuatayo katika Jiji kukosa Maji:
MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, KIBANGU, MAKUBURI PAMOJA NA ENEO LOTE LA TABATA.
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

0 comments:

Chapisha Maoni