Jumatano, Januari 06, 2016

TANZANIA KUWASAKA NA KUWATIMUA WAGENI WALIOSHIKA NAFASI ZA KAZI BADALA YA WAZAWA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema kuwa imepokea malalamiko kutoka kwa watanzania kupitia vyanzo mbalimbali kutokana na hali ya kuwepo kwa wageni waliokuja hapa nchini na kujipa nyadhifa mbalimbali katika makampuni, viwanda na mahoteli na kutumia vyeo vyao vibaya kwa kuwanyanyasa wananchi. 
Kutokana na malalamiko hayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeiagiza idara ya uhamiaji kuwasaka wageni hao na kuwafukuza nchini mara moja. 
Pamoja na hayo, serikali ya Tanzania imetoa wito kwa watanzania ama raia wema kutoa ushirikiano na idara ya uhamiaji ili kuwafichuwa wageni hawa popote walipo ili zoezi hili likamilike kwa haraka.

0 comments:

Chapisha Maoni