Alhamisi, Januari 28, 2016

TAARIFA YA KUWALAZIMU WANAUME WA ERITREA KUOA WAKE WAWILI HAIKUWA YA KWELI

Taarifa iliyoazagaa kwenye mtandao kuwa Eritrea imewataka wanaume wa nchi hiyo kuoa wake wawili au vinginevyo kukabiliwa na kifungo cha jela, imekasirisha maafisa wa nchi hiyo. 
"Hata mtu mwendawazimu mjini Asmara atafahamu kuwa hiyo ni taarifa ya uongo," afisa mmoja wa Eritrea amesema' 
Taarifa hiyo ya uzushi iliandikwa kwenye tovuti moja ya Kenya iitwayo Crazy Monday. Wanaume kadhaa kwenye mitandao na hasa Twitter walisema wapo tayari kwenda Eritrea kuanza maisha mapya huko.

0 comments:

Chapisha Maoni