Alhamisi, Januari 21, 2016

S/KUSINI YAPATA HASARA KWA KUSHUKA BEI YA MAFUTA

Kuporomoka bei ya mafuta katika soko la dunia kulikosababishwa na njama na ukwamishaji wa kila namna wa Saudi Arabia, kumezisababisha madhara makubwa nchi zinazouza mafuta nje ikiwemo Sudan Kusini.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kutoka Nairobi, mji mkuu wa Kenya kwamba, Wizara ya Mambo ya Nje wa Sudan Kusini imeiomba Sudan zifanye tena mazungumzo ili kujadiliana kiwango cha mafuta ambacho kila nchi itakuwa na haki ya kusafirisha kupitia mabomba ya mafuta.
Serikali ya Sudan Kusini inazidi kupata hasara kutokana na kuwa, kila pipa moja la mafuta yake linanunuliwa kwa dola 20, yaani kwa upungufu wa dola saba ikilinganishwa na bei ya "Mafuta ya Brent" katika soko la Ulaya.
Mafuta ya Sudan Kusini yananunuliwa kwa bei hiyo ya chini kabisa katika hali ambayo gharama za kusafirisha kila pipa moja la mafuta ya nchi hiyo ni dola 24.
Hii ina maana ya kwamba, serikali ya Sudan Kusini inapata hasara ya dola nne kwa kila pipa la mafuta inalolisafirisha nje, suala ambalo limeleta wasiwasi wa kufungwa tena uzalishaji mafuta nchini humo.

0 comments:

Chapisha Maoni