Serikali ya Tanzania itapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuwa inachangia uharibifu wa mazingira
Waziri wa Mazingira wa Tanzania,January Makamba alisema kuwa ameagiza maafisa katika baraza la taifa linalosimamia mazingira (NEMC) kuandaa mpango maalum utakaofuatwa katika utupaji wa takataka za plastiki nchini humo.
"Kwanza tunataka kufanya utafiti na kuelewa mbinu bora za kushughulikia matumizi ya mifuko ya plastiki na wanunuzi," alisema huku akiongeza kuwa wataomba ushauri kutoka Rwanda ambao wamefanikiwa katika sekta hiyo.
Mifuko ya nailoni ilimepigwa marufuku nchini Rwanda tangu mwaka wa 2008




0 comments:
Chapisha Maoni