Uhuru wa Sheikh Issa Ponda umeingia katika sura nyingine kufuatia uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro, ulioumuachia huru kiongozi huyo wa dini aliyekuwa anakabiriwa na mashataka ya uchochezi.
Hata hivyo, alieleza kuwa bado upande wa mashtaka haujapewa nakala ya hukumu hiyo ingawa wameanza kuiomba muda mrefu uliopita, kitu ambacho amedai kinawashangaza.
“Hatujui kuna tatizo gani, maana tunapoomba kupatiwa nakala ya hukumu, hakimu amekuwa anatuambia kwamba bado hawajamaliza kuichapa, kwa kweli hii inashangaza,” Alisema.
Sheikh Ponda na wenzake waliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Novemba 30 mwaka jana baada ya kutowakuta na hatia katika makosa ya uchochezi na kukiuka amri ya mahakama. Kesi ambayo ilianza kusikilizwa tangu Mwaka 2013.
Chanzo: Dar 24



0 comments:
Chapisha Maoni