Jumapili, Januari 24, 2016

AJALI YA BASI LA ADVENTURE NA NOAH IMEUA WATATU

Taarifa ambayo tumeipata ni kuwa kuna watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya toyota Noah yenye namba za usajili T 243 DGB lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Tabora kugongana uso kwa uso na basi la abiria la kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T 852 CBF lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam katika kijiji cha Buingiri madukani wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

0 comments:

Chapisha Maoni