Jumatano, Januari 13, 2016

ADONDOKA TOKA GHOROFANI, ACHOMWA VIBAYA NA NONDO LAKINI AKANUSURIKA KIFO

MTOTO wa miaka 10, Aman Vishwakarma amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya nne hadi chini kisha kuchomwa na nondo huko Uttar Pradesh nchini India.
Inasemekana kuwa, Aman alipatwa na mkasa huo alipokuwa juu ya paa la ghorofa hiyo (ambapo ni nyumbani kwao) akifanya usafi ndipo akadondoka na kuchomwa na nondo yenye urefu wa futi nne, iliyozama kuanzia kwenye mgongo na ikatokeza kwenye makalio huku nondo hiyo ikikosa kidogo tu kuchoma kwenye uti wa mgongo wa mtoto huyo.
Aman anayetokea katika Wilaya ya Kaushambi mjini Uttar Pradesh nchini humo, amepona baada ya kufanyiwa upasuaji kwa saa nne na madaktari bingwa wa hospitali ya Narayan Swaroop waliofanya kila juhudi za kukitoa kipande hicho cha nondo na kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Madaktari wamesema, ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa nondo hiyo ilichana mshipa wake mkuu wa damu, kudhuru uti wa mgongo na mapafu pia hivyo kusababisha lita 2 za damu kuvujia kwenye tumbo la chakula.

0 comments:

Chapisha Maoni