Alhamisi, Januari 08, 2015

UKWELI WA MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEBAKWA HADI KUFA MBEYA


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Elika Mkumbwa( 8)amekutwa maekufa katika jumba bovu (pagale) eneo la Mtaa wa Ilomba Village.

Akizungumzia tukio hilo Balozi wa mtaa huo Ndugu Ezekiel Mwakalundwa amesema kuwa amepata taarifa za kupatikana kwa mwili wa mtoto huyo majira ya saa 1 na nusu asubuhi kutoka kwa majirani waliokuwa karibu na eneo.
Amesema baada ya kupata taarifa hizo aliongozana na majirani pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu huyo hadi eneo la tukio ambako kitendo hicho cha kikatili I,mefanyika na kukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa ndani ya sinki la kuogea ndani ya moja ya chumba kwenye pagale hilo huku ukiwa hauna nguo.
Amesema mara baada ya kuupekua mwili huo waligundua kuwa mtoto huyo aliofanyiwa vitendo vya kikatili kuwa alibakwa ambapo sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibika bibaya na tayari mwili wake ulianza kuharibika na kuanza kutoa harufu.
Amesema mara baada ya kushuhudia tukio hilo alitoa taarifa katika kituo cha polisi kati ambapo polisi walifika na kuchukua mwili wa marehemu huyo ma kupeleka katika hospital ya rufaa kwa ajili ya kuafanyiwa uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.
Amesema kutokana na mazingira yaliyonekana katika eneo hilo huenda binti huyo alibakwa hadi kufa kwani sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibika vibaya.
Kwa upande wao majirani wanao ishi karibu na eneo hilo wamedai kuwa tukio la kuwawa kwa mtoto huyo si tukio la kwanza kwani matukio ya aina hiyo yamewahi tokea zaidi ya mara tatu yakihusisha kubwakwa kwa watoto wadogo.
Mmoja wa majirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Kristina Mwakalundwa amesema tukio hilo ni la tatu kutokea ambapo kuna mapagara pamoja na miti ya mianzi ambayo ndio imekuwa chanzo cha kufanyikakwa matuki hayo ya ubakaji.
Amesema chanzo kingine cha tukio hilo kunatokana na baadhi ya wananchi kupanda mahindi pembezoni mwa makazi ya watu ahali ambayo imekuwa ikichangia kwa kiwango kikubwa kutoa mianya ya wahalifu kufanya vitendo vya kinyama vinavyo fanana na tukio hilo .
Kufuatia tukio hilo ameitaka serikali pamoja na wakazi wa eneo hilo kuungana kwa pamoja kuhakikisha wanapinga hatua ya baadhi ya watu kuendeleza shughuli za kilimo pembezoni mwa makazi ya watu.
Akizungumzia kwa masikitiko makubwa mama mlezi wa mto to huyo Ndugu Sala Mwandobo amesema binti yake alitoweka nyumbani toka jana January 7 mwaka huu nakwamba aliaga nyumbani kuwa anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji mita kadhaa toka nyumabni anako ishi mtoto huyo.
Akielezea zaidi mama huyo amesema kuwa yeye alikuwa safari na kwamba alirudi jana hiyohiyo ambapo mara baada ya kurudi nyumbani alimkuta binti huyo akiwa na sare za shule majira ya saa 9 mchana baada ya kulejea kutoka shule ambapo mtoto huyo alikunywa chai kisha kumuomba mama yake kuwa anataka kwenda kufua nguo kwani zimeloa ambapo alimruhusu na kumtaka awahi kurudi nyumbani .
Amesema baada ya mtoto huyo kuondoka alichukua muda mrefu hali ambayo ilizua hofu nyumbani kwako ambapo mama huyo aliagiza wenzankle kumfuata ikiwa majira ya saa 11 jioni ambapo hata hivyo hawakuweza kufanikiwa kumpata hivyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi ilomba majira ya saa 1 jioni .
Amesema baada ya kutoa taarifa hizo kituo cha polisi waliendelea kutoa taarifa pia kwa majirani huku wakiendelea kumtafuta hadi ilipo fika midaa ya saa6 usiku ambapo walikata taamaa na kurudi nyumbani.
Amesema ilipo fika asubuhi ya leo majira ya saa1 asubuhi walipata taarifa za kukutwa kwa mtoto akiwa amekufa ndani ya pagale jirani na nyumbani kwao.
Amesema baada ya kwenda kushuhudia mwili huo waligundua kuwa ni mtoto wake ambapo alikutwa akiwa na ndoo pamoja na nguo alizokwenda kufua huku akidai kuwa yawezekana watu hao waliofanya kitendo hicho walimkamatia maeneo hayo kabla ya kufika eneo la kufulia nguo.
Amesema inasikitisha sana na inamuuma sana kwani binti huyo alimchukua kwa mdogo wake kijijini akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu akiwa katika hali mbaya ya kiafya ambapo mapaka sasa umauti unamkuta mtoto huyo
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa motto huyo umehifadhiwa katika hospital ya rufaa mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni