Iko hivi,....Mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa wa nchini Marekani mwenye asili ya Afrika Dr.Robert Shumake amekubali kuzileta treni za kisasa katika jiji la Dar es salaam ili kusaidia kutatua kero ya usafiri katika jiji hilo ambapo anatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni arobaini kufanikisha hilo muda wowote kuanzia sasa.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano ya uletaji wa treni hizo Dr.Shumake amesema anatarajia treni hizo zitafanya kazi saa ishirini na nne na anaisubiri serikali ya Tanzania imalize tathmini ya gharama za mradi huo na yeye aweze kutoa fedha za kuufanikisha.

Naye waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema treni hizo zitafanya kazi kati ya Stesheni na Pugu na zitatumia miundombinu ya reli iliyopo ila kutakuwa na ujenzi wa reli zingine katika baadhi ya sehemu kuruhusu treni kupishana.
Sasa mkitaka kujua kama huu ni ufisadi wa kutisha ambao Mwakyembe amesign huko USA na unafana na ule wa upanuzi Bandari uliomfukuzisha kazi Omari Nundu baada ya kuuweka wazi.
Nimepitia mtandao wa wizara ya mwakyembe lakini cha ajabu hakuna details zozote za kuonyesha kinachoendelea na maswali yamekuwa mengi zaidi kuliko majibu:
Nimepitia mtandao wa wizara ya mwakyembe lakini cha ajabu hakuna details zozote za kuonyesha kinachoendelea na maswali yamekuwa mengi zaidi kuliko majibu:
1. Je tenda ya Feasibility ya huu mradi Ilitangazwa lini na wizara?
2. Je vigezo vipi vilitakiwa ili makampuni yapitishwe?
3. Kampuni zilizo bid ni zipi ?
4. Kampuni zilizo ondolewa ni zipi na kwa vigezo vipi?
5. Kampuni zilizokuwa shorlisted ni zipi?
6. Kampuni iliyoshinda ni ipi? na walishinda kwa vigezo vipi?
7. Tenda ya kufanya hii kazi ilitangazwa lini?
8. Masharti yepi yalikuwa ili kampuni ipewe contract?
9. Kampuni zipi zilibid?
9. Zilizoondolewa zilikuwa zipi?
10. Hii kampuni ilikuwa awarded lini?
11. Ripoti ya Environmental Impact Assessment iko wapi na inasemaje?
12. Je Mwakyembe na jamaa zake pale wizarani walifanya due diligence kwa hii kampuni ya kitapeli?
13. Ofisi ya Mheshimiwa Rais ilikuwaje hawakufanya vetting kabla hawajamwingiza Rais kwenye huu upuuzi wa kusign na matapeli?
14. Kwa nini wizara ya mwakeyembe haitaki kuweka wazi hizi documents au inapingana na juuhudi ya OPEN GOVT INITIATIVE ya JK?
15. Kwa nini Mwakeyembe na wizara yake hawataki kuweka wazi INFRASTRUCTURE STRATEGIC PLAN ya Tanzania? Wanaficha nini?
16. Kwa nini serikali haijafanya consultation na wananchi wanaoishi maeneo ambayo hizo treni zitapita ?
0 comments:
Chapisha Maoni