Mashabiki wa klabu ya Galatasaray walilazimika kutulizwa kwa vitisho
baada ya kupandwa na jazba kufuatia timu yao kufanya ovyo wakati wa
mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo na kujikuta wakifungwa mabao manne
kwa moja dhidi ya Arsenal.
Kikosi cha usalama cha uwanja wa Emirates kililazimika kuingiza mbwa
uwanjani mara baada ya mchezo huo kumalizika kutokana na mashabiki hao
kutoka nchini Uturuki kurusha mafataki katika sehemu ya kuchezea ikiwa
ni ishara ya kuchukizwa na matokeo.
Askari wa kikosi cha usalama cha uwanja huo kililazimika kusimama
mbele ya mashabiki huku kikiwa na mbwa wakali na kuwataka mashabiki wa
Galatasaray kutoka uwanjani kwa utaratibu na amani.
Hata hivyo mashabiki wa Galatasaray, walitupa mafataki wakati mchezo
ukiendelea hatua ambayo ilimfanya kiungo mshambuliaji kutoka nchini
Uholanzi Wesley Sneijder kuwatuliza.
Kufuatia matokeo ya usiku wa kuamkia hii leo klabu ya Galatasaray
inaendelea kuwa na point moja katika msimamo wa kundi la nne ambalo
linaongozwa na Borussia Dortmund wenye point sita baada ya kushinda
michezo yao miwili, wakifuatiwa na Arsenal wenye point tatu na klabu ya
Anderlecht ya nchini Ubelgiji imefungana point na waturuki.
0 comments:
Chapisha Maoni