Jumatano, Oktoba 01, 2014

TAZAMA CHRISTIANO RONALDO FEKI ANAVYOTESA MITAANI

Akionekana ni mwenye ngozi nyororo na umbo lenye mvuto kama mshambuliaji wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, kijana anaetambulika kwa jina Joe Weller, amekua akiwahadaa wasichana kwa kujifafanisha na Cristiano Ronaldo.
Kijana huyo amekuwa akifanya matukio ya kuwahadaa watu hususana wasichama, katika mji wa Brighton uliopo kusini mwa Uingereza ambapo mara kadhaa wasichana wamekua wakivutiwa nae na kufikia hatua ya kumtamani kutokana na mvuto wake.
Hata hivyo wasichama wengi wamekuwa wakiamini kijana huyo ndio Ronaldo wa ukweli, kutoka kwenye klabu ya Real Madrid kwa namna anavyovaa na muonekano wake na pia hutumia matamshi ya maneno ya lugha ya kireno.
Mbali na hivyo wasichama wengine hufika mbali zaidi kwa kutaka kumbusu na kumkumbatia ikiwa ni sehemu ya kutaka kuonyesha hisia zao kimapenzi kwa Cristoano Ronaldo ambaye inasemakana hupata wakati mgumu anapokutana na wakinadada mitaani.

0 comments:

Chapisha Maoni