Katika siku kama ya leo miaka
1375 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Imam Hussein bin Ali (AS),
mjukuu wa Mtume SAW aliondoka Makka na kuelekea Kufa nchini Iraq baada
ya kukataa kumbai na kutoa kiapo cha utiifu kwa Yazid bin Muawiya. Miezi
minne kabla ya hapo, Imam Hussein alikuwa amewasili mjini Makka akiwa
pamoja na familia yake na alikitumia kipindi cha kuweko waumini
waliotoka katika pembe mbalimbali za dunia kwa ajili ya kufanya ziara
katika nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu, kuwaamsha na kuwabainishia dhulma
na ufisadi mkubwa uliokuwa ukifanywa wa utawala wa Yazid mwana wa
Muawiya. Wakati huo huo kutokana na wito wa mara kwa mara wa watu wa
Kufa na njama za utawala wa Yazidi za kutaka kumuuwa, Imam Hussein
aliondoka Makka na kueleka Kufa.
Miaka 82 iliyopita katika siku
kama ya leo Iraq ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni Mwingereza. Iran
iliiweka Iraq chini ya mamlaka yake mwaka 539 kabla ya kuzaliwa Nabii
Issa (A.S). Iraq ilikuwa sehemu ya utawala wa kifalme wa Iran hadi ardhi
hiyo ilipokombolewa na Waislamu mwaka 642 Miladia. Iraq iliendelea
kudhibitiwa na utawala huo wa kifalme hadi mwishoni mwa utawala wa Bani
Ummaya na mji wa Baghdad ukachaguliwa kuwa makao makuu sambamba na
kuingia madarakani utawala wa Abbasiya.
Na miaka 36 iliyopita katika
siku kama ya leo, baada ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu kuzuiwa
kuendesha shughuli za kisiasa na kidini huko Iraq, mwasisi huyo wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliamua kuondoka Iraq na kuelekea Kuwait.
Hata hivyo serikali ya Kuwait ilimzuia Imam kuingia nchini humo ili
kulinda uhusiano wake na utawala wa Shah. Kufuatia hatua hiyo, Imam
Khomeini siku kadhaa baadaye alielekea nchini Ufaransa. Ni vyema
kuashiria hapa kuwa, miamala na vitendo visivyo vya kibinadamu vya
utawala wa Baath wa Iraq dhidi ya Imam Khomeini vilizusha hasira za
wananchi wa Iran, ambao walikuwa katika kipindi nyeti cha kupambana na
utawala dhalimu wa Shah hapa nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni