Kampuni moja nchini China
inakabiliwa na tisho la kutozwa kiwango kikubwa cha faini kwa kuwakodi
wanawake kuvua nguo zao kwenye treni mjini Shanghai kwa lengo la
kutangaza biashara ya kampuni hiyo kwa abiria.
Katika moja ya
video iliyowekwa kwenye mtandao wiki jana, wasichana wawili ghafla
walianza kuvua nguo zao na kusalia na nguo za ndani pekee katika treni
hiyo iliyokuwa imejaa watu.
Abiria walionekana wakirekodi wasichana hao kwa simu zao za viganjani lakini mwanamke mmoja wa makamo aliwakaripia sana.
Mwanamume
mmoja kutoka katika kampuni ya huduma za dobi ambayo wasiahana hao
walikuwa wakiitangaza, naye alionekana akiokota nguo za wasichana hao
walizokua wanavua.
Baada ya filamu ya wasichana hao wakivua nguo
kuenea mitandaoni, polisi waliwasiliana na kampuni hiyo kujibu
walichokuwa wanakifanya.
Kampuni hiyo inayotoa huduma za dobi ,kwa
jina 'Tidy Laundry', ilipoona ikipata sifa mbaya, iliamua kuomba radhi
kwa kosa hilo ikisema kuwa ilinuia tu kutangaza huduma zake kwa wabiria
waliokuwa ndani ya treni hiyo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Shanghai Daily.
Wamiliki wa kampuni hiyo, wanasema kila aliyehusika kwenye tukio hilo alikuwa muigizaji aliyekuwa amekodiwa.
Hata
hivyo huu bila shaka sio mwisho wa masaibu ya kampuni hiyo-polisi
wanasema wanachunguza ikiwa ilivunja sheria zinazopiga marufuku
matangazo ya kibiasga ambayo yanakera jamii.
0 comments:
Chapisha Maoni