KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA RAI YOHANA MWENYE UMRI WA MIAKA 04, MKAZI WA RUJEWA WILAYA YA MBARALI AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO MJI MDOGO, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA, MAREHEMU ALIKUWA AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE JIRANI NA KISIMA HICHO CHA MAJI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI KUJIEPUSHA NA MATUKIO KAMA HAYA. AIDHA, ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYO WAZI PAMOJA NA MITARO KWANI NI HATARI KWA WATOTO.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTOTO MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA RAI YOHANA MWENYE UMRI WA MIAKA 04, MKAZI WA RUJEWA WILAYA YA MBARALI AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO MJI MDOGO, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA, MAREHEMU ALIKUWA AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE JIRANI NA KISIMA HICHO CHA MAJI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI KUJIEPUSHA NA MATUKIO KAMA HAYA. AIDHA, ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYO WAZI PAMOJA NA MITARO KWANI NI HATARI KWA WATOTO.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 08 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AMBAO NI 1. ESIDO HANDSON (20) 2. TAKIRE AMIRO (16) 3. TESHAR ZENDEKAR (18) 4. NDEKERO ABDULLY (18) 5. ISAGAR WOCHAM (20), 6. DIRAMO MITORO (22) 7. AMBANYA ABICHO (24) NA 8. TARAFA ACHISHO (24).
WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 20:30 USIKU HUKO ENEO LA BAGAMOYO, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAGENI NA WAHAMIAJI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA KISHERIA ZA KUINGIA NCHINI. AIDHA, ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MKAZI MMOJA WA KAPWILI WILAYA YA KYELA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KENEDY CHENGULA (19) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA DOUBLE PUNCH KATONI 06 NA BWANA JIN KATONI 02.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA TENENDE, KATA YA TENENDE, TARAFA YA NTEBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA ANATOKEA NCHI JIRANI YA MALAWI AKIWA NA POMBE HIZO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII NA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA BINADAMU.
KATIKA MSAKO WA TATU:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ANASTAZIA TUNYANDE (24) MKAZI WA NZOVWE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] PAMOJA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 12.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA BAADA YA KUPEKULIWA NYUMBANI KWAKE NA KUKUTWA NA MTAMBO HUO PAMOJA NA POMBE HIYI HARAMU.
AIDHA, WAKATI HUO HUO MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BONIFACE ERICK (25) MKAZI WA UYOLE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 01.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA WAKATI AKIWA ANAKUNYWA POMBE HIYO KWENYE KLABU CHA POMBE ZA KIENYEJI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHINI.
KATIKA MSAKO WA NNE:
WATU WAWILI WAKAZI WA MAJENGO JIJINI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. GODFREY MBASHA (19) NA 2. OBOKELA GWAKISA (21) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAMU 50.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MAJENGO, KATA YA MAJENGO, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. BHANGI HIYO ILIKUWA IMEFICHWA NDANI YA NYUMBA YA WATUHUMIWA HAO AMBAO NI MTU NA MKE WAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHINI.
0 comments:
Chapisha Maoni