Jumanne, Oktoba 21, 2014

MAD ICE: MKITO INALIPA ZAIDI KULIKO iTUNES

Mwimbaji Mad Ice amezipima njia mbili za uuzaji wa nyimbo za wasanii kwenye mitandao, iTunes (Kimataifa) na Mtandao wa Mkito ambao ni maalum zaidi kwa wasanii wa Afrika Mashariki.
Mad Ice ameweza kupima baada ya kutumia muda mrefu njia ya iTunes na hivi karibuni kutumia mtandao wa Mkito.
Akiongea na tovuti ya Fichuo Tz Times Fm, Mad Ice amesema kuwa mauzo ya muziki kwa wasanii wa Afrika Mashariki ni rahisi zaidi na inalipa zaidi kupitia mtandao wa Mkito kuliko mtandao wa iTunes.
Mimi nafikiri locally mtu ambaye ameweka Mkito ni mtu ambaye amekuja kuokoa wasanii wa kizazi kipya. Hata sio kizazi kipya tu yaani local artists ni mtu ambaye amewawekea platform ambayo ni ya maana zaidi hata kuliko iTunes
ameeleza Mad Ice
Kwa sababu muziki wangu uko iTunes miaka mingi. Kuanzia 2006/2007 muziki wangu unapatikana kwenye all major digital stores. Lakini unajikuta kwamba kama hauna major airplay kwenye major radio stations mbalimbali kubwa duniani watu hawatakufahamu mapema, watu wa nje. Na ile ni kwamba unakuta ni watu wan je ambao wanafahamu sana kuhusu iTunes. Locally hapa mtu utakuta anakwambia mimi siwezi kutumi iTunes kwa sababu mbalimbali.
Mad Ice amewashauri wasanii wengine kujiunga na mtandao wa Mkito ili kufaidika zaidi na nyimbo zao huku akisifia njia ya uwazi inayotumika kuuza nyimbo kupitia mtandao huo.

0 comments:

Chapisha Maoni